UTANGULIZI

Wachagawote ni Jukwaa huru la Kidijitali linalowaunganisha Wachaga wote waliopo ndani na nje ya Tanzania kupitia taarifa, historia, utamaduni, matukio na masuala yanayogusa maisha ya jamii ya Kichaga kwa ujumla

Jukwaa hili lipo kama daraja la mawasiliano na utambulisho wa pamoja wa Wachaga katika ulimwengu wa kisasa wa kidijitali
.



🟢 SISI NI NANI?

Wachagawote si umoja, si chama, wala si kikundi cha wanachama.
Ni jukwaa wazi linalotumika kukusanya, kuchuja na kusambaza taarifa zinazohusu Wachaga bila upendeleo.

Jukwaa hili lilianzishwa kama blogu ya kijamii kwa lengo la kutoa nafasi kwa Wachaga kushirikishana mawazo na taarifa. Kadri mahitaji ya jamii yalivyoongezeka, Wachagawote ilikua na kupanuka kuwa jukwaa pana la kidijitali kupitia tovuti na mitandao ya kijamii.

Leo, Wachagawote ni sauti ya pamoja ya Wachaga inayojikita katika:

  • Utambulisho

  • Elimu ya Jamii

  • Mshikamano

  • Maendeleo ya Pamoja


🟢 DHAMIRA YETU

Dhamira ya Jukwaa la Wachagawote ni:

  • Kuunganisha Wachaga popote walipo duniani

  • Kutoa na kusambaza taarifa sahihi zenye manufaa kwa jamii

  • Kuenzi na kuhifadhi historia, mila na utamaduni wa U-Chagga

  • Kuhamasisha mawazo chanya na mshikamano wa kijamii

  • Kutoa nafasi ya kutangaza matukio, fursa na shughuli zinazowahusu Wachaga



🟢 JINSI JUKWAA LINAVYOENDESHWA

Jukwaa la Wachagawote linaendeshwa kwa misingi ifuatayo:

  • Ni jukwaa huru lisilo la kisiasa

  • Halikusanyi ada za uanachama

  • Halina usajili wa wanachama

  • Halina kamati au uongozi wa kimuundo

  • Haliko chini ya taasisi, chama au umoja wowote

Maudhui yanayochapishwa huchujwa kwa kuzingatia ukweli, heshima na maslahi mapana ya jamii ya Wachaga.