Utambulisho wa Wachagawote
Jukwaa la kijamii linalojikita katika kuunganisha Wachaga duniani kote kupitia mifumo shirikishi yenye uwazi na uwajibikaji.
Wachagawote
Si chama, si biashara, wala si taasisi ya kisiasa. Ni jukwaa huru la kidijitali linaloendeshwa na wanajamii kwa lengo la kuhifadhi utamaduni, kuimarisha mshikamano, na kuchochea maendeleo ya pamoja.
Zaidi ya wanajamii 8,200+
Washiriki hai katika mifumo mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.
Majadiliano ya Kila Siku
Taarifa na mawazo yanashirikishwa kwa wakati halisi kupitia majukwaa yetu.
Mifumo ya Kijamii
Sisi kwa Sisi, Ushira, na mifumo mingine shirikishi ya kuimarisha ushirikiano.
Dira na Dhamira
Malengo yetu ya muda mrefu na msingi wa kuwepo kwetu
DIRA YETU
Kuwa jukwaa linaloongoza kwa kuwaunganisha Wachaga duniani, kuhifadhi utamaduni wetu tajiri, na kujenga jamii yenye mshikamano imara na maendeleo endelevu.
DHAMIRA YETU
Kuunda mfumo shirikishi unaowawezesha Wachaga kubadilishana uzoefu, maarifa na rasilimali kwa lengo la kuinua hali ya maisha ya kila mmoja na jamii kwa ujumla.
Maadili Yetu
Kanuni zinazotuongoza katika kila tunachofanya
Uwazi
Taarifa zote zinazohusu jukwaa na shughuli zake huwasilishwa kwa uwazi kwa wanajamii wote bila kuficha chochote.
Uwajibikaji
Kila mshiriki anawajibika kwa matendo yake na kuzingatia makubaliano ya jumuiya kwa nidhamu na uaminifu.
Mshikamano
Tunashirikiana na kusaidiana katika nyakati zote, kwenye shida na raha, kama jamii moja iliyoungana.
Usalama
Taarifa za wanajamii zinalindwa kwa usalama wa juu na hazitumiwi nje ya mfumo bila ridhaa ya mhusika.
Nidhamu
Kuzingatia muda na makubaliano ni nguzo muhimu katika mifumo yetu yote ya kijamii.
Ushirikiano
Tunaamini katika nguvu ya pamoja na kushirikiana kwa hiari bila kulazimishwa.
Nguzo za Ushirikiano
Kupitia mifumo ya kijamii iliyo wazi na ya hiari, Wachagawote inaimarisha mshikamano na uwajibikaji miongoni mwa wanajamii.
Mpango wa Sisi kwa Sisi-DSM
Mfumo wa kijamii unaosimamiwa kwa uwazi, nidhamu na uwajibikaji. Washiriki huchangia kwa hiari na kupokea kwa muda maalum.
Soma ZaidiUmoja wa Shida na Raha (Ushira)
Umoja wa kijamii unaolenga kusaidiana katika shida na mafanikio. Wanajamii hukusanyika kusaidiana katika matukio mbalimbali.
Tembelea UshiraWhatsApp Community
Jiunge na majadiliano na upate taarifa kwa wakati halisi. Jumuiya yetu ya WhatsApp ina wanachama zaidi ya 350+.
Jiunge SasaJukwaa Linalokuwa
Tunajivunia kuwa na jamii inayokua kwa kasi na ushirikiano imara
Mpango wa Sisi kwa Sisi
Mkombozi wa kiuchumi kwa akina mama na vijana wenye maono ya mafanikio.
Mkombozi wa Akina Mama
Inawapa akina mama uwezo wa kupata mitaji ya mzunguko kila siku bila riba wala masharti magumu, kukuza biashara zao na kuleta heshima ndani ya familia kupitia mshikamano.
Mtaji kwa Vijana
Sisi kwa Sisi inageuza mzunguko wa siku 100 kuwa daraja la vijana kuanzisha miradi mipya. Ni shule ya nidhamu ya kifedha inayokuandaa kuwa mfanyabiashara mkubwa wa kesho.
Ukuaji wa Pamoja
Wanachama wanapata uwezo wa kufanya uwekezaji ambao peke yao isingekuwa rahisi. Huu ni mkakati wa dhati wa kukuza mzunguko wa pesa (Cashflow) kwa kila mwanajamii.
Jiunge na Wachagawote Leo
Kuwa sehemu ya jamii inayothamini utambulisho, mshikamano na maendeleo ya pamoja.