Dr. Habel Noah kupitia ukurasa wake wa fecebook ametukataza kutupa mbegu ya parachichi kila tunapokula tunda hilo kwani mbegu ina faida nyingi kiafya zaidi ya tunda lenyewe.
Anasema kwamba Amino acids zinazopatikana kwenye tunda lake zinapatikana kwa asilimia 70% zaidi kwenye mbegu.
Ametutajia faida mbalimbali tutakazozipata kwenye mbegu za parachichi kama ifuatavyo;
1. Inazuia seli za mwili kuzeeka mapema.
2. Inazuia kupata magonjwa ya moyo.
3. Inaongeza kinga ya mwili kupambana na magonjwa mbalimbali.
4. Ni msaada kwa watu wanaotaka kupunguza uzito, husaidia kuchoma mafuta ya mwili.
5. Kutibu matatizo ya kuharisha na magonjwa mengine ya tumbo.
6. Unaweza kuitumi kwa kuongeza hamu ya tendo la ndoa. (kwa Wanawake pia husaidia kuongeza joto kwa Bibi)
7. Huondoa matatizo ya kuuma kwa misuli na joints.
8. Ni msaada kwa afya ya ngozi.
9. Unaweza kuituma kutibu pumu (Asthma).
10. Inazuia kifafa.
JINSI YA KUITUMIA:
Kwanza ondoa gamba lake laini juu ya mbegu Iitwange.
Ukisha twanga weka maji uchemshe kwa dakika 10. (Maji unaweka kulingana Na wingi wa mbegu ulizotumia, isiwe nzito sanaa)
Kisha iache kwa dakika tano ipoe na pia ili mchanganyiko huo utulia kwa ajili ya kupata juisi yake.
Dr. Habel ameshauri tuitumie kunywa kama juisi mara baada ya kupata chakula.
Haya ndugu yangu, wewe ulikuwa kama mimi ninayetupa mbegu za parachichi bila kufahamu faida zake? Aisee mimi baada ya kupata elimu hii kutoka kwa Dr. Habel, nimeamua naanza leo kunywa juisi hii kama tiba kwangu, wewe je?
Hebu niwekee comment yako hapa chini.
Usisahau kushare kwa wengine nao waipate elimu hii.