Baadhi ya Wachaga wanasema, "...Kunywa Mbege sio 'Dhambi'...''

 




Katika kupitapita mtandaoni, nikakutana na mwandishi fulani ameelezea kwa kifupi sana kuhusu mbege, nimesoma na nikaona nikuwekee na wewe ujisomee mwenyewe kisha unipe maoni yako kuhusu unywaji wa mbege kwa kabila letu Wachaga.

Aliandika hivi...

'''Mbege''' ni pombe ya asili ya Wachaga, wakazi wa mkoa wa Mkoa wa Kilimanjaro.  Mbege hutengenezwa na ndizi mbivu, ulezi, na maji. Mara nyingi mbege hutengenezwa na wanawake na hutumika katika sherehe na matukio mbalimbali kama vile harusi, misiba, [[ubarikio]], kuzaliwa kwa mtoto, n.k. Mbege hutumiwa pia kama faini kwenye mahakama za jadi. Utengenezaji wa mbege hufanywa pia kama shughuli ya kibiashara. Mbege huuzwa katika vilabu vya pombe na pia majumbani.

Pombe hii hutengenezwa kwa kuchemsha ndizi mbivu kama vile [[ndizi songea]], [[ndizi uganda]],kibungara,kisukari(kama zinapatikana kwa sana) n.k. Ndizi hizo zikishachemshwa huachwa kwa kipindi cha kama tatu au zaidi ili zichache. Baada ya hapo unga wa ulezi hupikwa na kuachwa upoe. Ndizi zilizochemshwa na kuchacha huchanganywa na maji kisha kukamuliwa ili kupata juisi yake. Juisi hiyo huchanganywa na unga wa ulezi uliopikwa na tunapata (kivuo, kifue, togwa) na kuachwa usiku mzima. Kesho yake mbege huwa tayari kwa kunywewa.

pombe hii kama haitanyewa na kumalizika siku huiyo basi ikilala tunapata kitu kinachooitwa ngera, ambayo ni chachu sana, ila ngera pia huweza kuzimuliwa na kuwa pombe ifaayo tena kwa kuchanganya na unga uliopikwa na unga kidogo usiopikwa, ila ngera ikilala tena humwagwa kwani haitafaa kunywea tena

Watengenezaji wengi wa pombe huwa wanaweka gamba la mti wa [[msesewe]], hasa maeneo ya kibosho,machame na rombo ili kuongeza ladha ya uchachu na kupunguza kasi ya mbege kuchacha.

Chombo maalum kiitwacho [[kata]] hutumiwa kunywea mbege, ila mara nyingi sehemu za mijini hutumia vyombo vya plastiki, vikiwa na ujazo tofauti navyo huitwa chubuku na kitochi. Katika maeneo ya vijijini mbege hunywewa kijamaa kwa kupokezana kata. Mtu mmoja anakunywa kisha anampatia mwingine anayekunywa na kumpa mwingine.

Akamaliza hivyo.


Nilipenda japo upitie tu hayo maelezo kwa ufupi kama nawewe ulikuwa ujui utakuwa umejua na kama ulikuwa unajua basi sio mbaya ukaongezea na haya pia.

Sasa njoo kwenye swali langu uniambie basi hapa kwenye comment yako, kuhusu hiyo kauli imeenea sana Uchagani kuwa kuhusu vilevi vilivyokatazwa tusinywe ili kuepuka kutenda dhambi kama ambavyo ni Pombe(Kilevi) wachaga wengi huku Moshi wamesema ukinywa Mbege sio 'dhambi' na isiwekwe kwenye hiyo orodha za vilevi ambavyo binadamu anapaswa kuviepuka katika kujenga mahusiano mema na Mungu.

Je, wewe unasemaje?
Niandikie hapo chini maoni yako...

Newer Post Older Post