Utambulisho na Maandalizi ya Waratibu wa Wachagawote Dar es Salaam umefanyika leo 06 March 2022

 


Ni Kikao cha Utambulisho rasmi kwa Wajumbe wanaoandaliwa kuwa Waratibu wa shughuli zote za Umoja wa Wachagawote Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika leo Tarehe 6 March 2022 maeneo ya Lego Bar iliyopo Barabara ya Shekilango Wilaya ya Ubungo majira ya Saa 04:03 Jioni hadi 06:52 Jioni.

Kikao hicho uliandaliwa na Muasisi wa Umoja wa Wachagawote Ndg. Rizikiel Mmari kwa kutoa taarifa kupitia Makundi ya Whatsapp ambako Ndg Mmari yeye ndio Admin wa Makundi yote mawili ya Wachagawote.

Utambulisho uliambatana kufamiana kwa wajumbe wao kwa wao pamoja na Muasisi huyo Ndg. Mmari kuelezea malengo ya kuanzisha Umoja wa Wachagawote na makusudio ya kuwaandaa Waratibu wa shughuli za Umoja wa Wachagawote. 

Ndg Mmari alieleza kuwa Umoja wa Wachagawote ni Umoja wa hiari unaoundwa na Wachagawote wenye Asili ya Old-Moshi, Kibosho, Machame, Rombo, Marangu na Siha na unalenga kuwanufaisha Wanaumoja(Wanachama) Kiuchumi na Kijamii.

Akitoa ufafanuzi Ndg Mmari alisema, Umoja utajikita zaidi kwenye kutoa suluhisho la matatizo na mahitaji yanayowakabili Wanaumoja huo haswa kuondokana na ile dhana aliyoiita ya Huruma Huruma na kuwa na mikakati ya uhakika kwa kila linapotokea hitaji kusewepo hali ya Kuoneana huruma ili kumsaidia Mwanaumoja bali iwe ni utaratibu rasmi kama umetokea msiba iwe Umoja wa Wachagawote unatoa kiasi kadhaa kwa mfiwa na sio swala la kusubiria michango au mwanaumoja huyo kutembeza bakuli la michango.

Akiendelea kueleza zaidi Mmari alisema imezoeleka kwenye vikundi vingi kunakuwa na michango ya aina ya kujitolea tu na wanakikundi kuwa na mazoea ya kuvuna tu bila kupanda kwenye mifuko ya kikundi jambo ambalo linavipelekea vikundi vingi kushindwa kufikia malengo na hatimaye kuvunjika.

Mmari amesema Umoja wa Wachagawote utajikita zaidi kuwatumikia wanaumoja na sio wanaumoja kutumikia Umoja wenyewe. Kwa kulithibitisha hilo Ndg Mmari alisema kabla ya kuwa na wazo la kuanzisha Umoja huo aligundua kuwa Maendeleo ya Umoja kama huu yanahitaji kuwa na misingi imara ya kiuchumi ya Umoja na pia kwa kila Mwanaumoja mwenyewe, hivyo anaona wazi Umoja huu utakuwa suluhisho rasmi kwakuwa umelenga kuwa na Uchumi imara kwa kila mwanaumoja na pia kwa Umoja wenyewe.

Wajumbe wote walionyesha kukubaliana na maono ya Ndg Mmari na walipata nafasi ya kumuuliza maswali Ndg Mmari na akayajibu kwa ufasaa na wao kuridhika. Pia walishiriki kwa kutoa mitazamo yao juu ya Umoja wa Wachagawote ambapo kati yao Dada Aika Kimario alisema, yeye anaona Umoja huu utakuwa mkombozi kwa Wachaga wengi kwakuwa yeye ni mwanamke aliyefanikiwa kumiliki nyumba yake mwenyewe kutokana na kuungana na vikundi vya kusaidia kibiashara na kwa jinsi anavyoona malengo ya Ndg Mmari ameongeza faida zaidi kwa Mwanaumoja na ingefaa kuungwa mkono na kila Mchaga. 

Kwa upande wake mjumbe mwingine Dada Thea Mbowe yeye anaona kama mipango imechelewa sana na anatamani mikakati ifanywe haraka ili ukombozi kwa Wachaga uanze kuonekana mapema kwa sababu anaona wazi ni Umoja ambao utakuwa ni Suluhisho kibiashara kwani umegusa maeneo sugu yanayohitaji kusaidiwa ukiwa kama Mwanaumoja.
Pia kwa upande wake mjumbe mwingine Ndg. Aloyce Soka yeye amesema anautabiria Umoja huu kuwa msaada mkubwa kwa kila Mwanaumoja haswa kuhusu kuwezeshana mitaji ya Biashara na kupatiwa masoko ya biashara. 

Pia walikuwepo wachangiaji wengine Ndg. Innocent Mushi yeye alisema ameona maboresho mengi ambayo hapo awali alipokuwa kwenye vikundi vingine alikutana na kasoro tofauti tofauti na aliwahi kuwa na hitaji la kupata kikundi kitakachogusa maisha ya Wachaga na anashukuru Mungu amekuwa mmoja wa waliobahatika kushirikishwa, ameahidi kuunga mkono na kuhakikisha Umoja huu wa Wachagawote unafikia malengo.

Kwa kumalizia Muasisi wa Umoja wa Wachagawote Ndg. Mmari alisema Umoja huu utaongeza chachu ya Maendeleo na kuimarisha Mshikamano kwa Wachagawote kwani umeonyesha njia sahihi ya Upendo na Mshikamano pia Usawa, pasipo Uchoyo na Ubinafsi mambo ambayo ni adui mkubwa wa Maendeleo(Uchoyo na Ubinafsi)

Pia Ndg. Mmari aliwashauri wajumbe kuwa na tabia ya kupenda kujitolea na kuhakikisha wanakuwa msaada kwa wengine pasipo kuendekeze maslahi binafsi au kuona shida ya mwenzio kama fursa ya kujipatia pesa.
Amesisitiza kuwa maendeleo yanapatikana baada ya kumsaidia mwingine na sio kuchuma kutoka kwa mwingine, ni vyema kupokea fadhila kuliko kupokea Malipo.

Utambulisho huo pia uliambatana na kupata chakula cha jioni ambapo wajumbe wote walishikiriana pamoja kula na Kufurahi kukutana na Muasisi wa Umoja wa Wachagawote Ndg. Rizikiel Mmari kama wanavyonekana kwenye picha hapo chini.












Newer Post Older Post