Ni kikao cha Kikundi cha Kijamii kinachoitwa Wachagawote kama ilivyo kawaida yao wamendelea na vikao vya kikundi na kwa mara nyingine tena kwa Mkoa wa Dar es Salaam kikao hiki cha Tatu (b) kilifanyika Tarehe 3 April 2022 maeneo ya Lego Bar iliyopo Barabara ya Shekilango Wilaya ya Ubungo majira ya Saa 05:00 Jioni hadi 08:00 Usiku.
Kikao hicho kiliandaliwa na Muasisi wa Umoja wa Wachagawote Ndg. Rizikiel Mmari kwa kutoa taarifa kupitia Makundi ya Whatsapp yote mawili(Wachagawote 01 pamoja na Wachagawote 02)
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwl. Thadey Kitaly ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wachagawote aliyotuandikia kupitia barua pepe...
Mwl. Thadey ameeleza kikao hicho kilikuwa na Agenda zifuatazo;
Kufungua kikao
Mahudhurio
Utambulisho
Taarifa fupi kuhusu kikundi cha wachaga wote
Taarifa fupi juu ya kikao kilichopita
Utekelezaji a maazimio ya kikao kilichopita
Mengineo
Kufunga kikao
KUFUNGUA KIKAO
Kikao kilifunguliwa na Ndg. RIZIKIEL MMARI ambaye ni Muasisi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wachagawote mnamo saa 11 kamili jioni kwa kukaribisha wajumbe na kuwashukuru kwa kuja kwenye kikao.
MAHUDHURIO
Kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe sita kama majina yao yanavyosomeka hapo chini;
RIZIKIEL MMARI ……………..MWENYEKITI
ALOYCE F. SOKA…………….MJUMBE
THADEY F. KITALY ………….. KATIBU
PIUS D KIWANGO …………..MJUMBE
INNOCENT H MUSHI ………. M/HAZINA MSAIDIZI
AVELINI V. MUSHI ……………MJUMBE
UTAMBULISHO
Utambulisho ulifanya kwa wajumbe kujitambulisha kwa majina yake na shughuli anayofanya na sehemu ya Uchagani alikotoka au kuzaliwa
TAARIFA FUPI JUU YA KUNDI LA WACHAGA WOTE.
Mwenyekiti Ndg. Mmari ambaye ndiye muasisi alitoa taarifa fupi kuhusu Umoja wa Wachagawote akaeleza muda ulipoanza changamoto alizokumbana nazo kwa mara ya kwanza tokea mwaka 2015 na hadi kufikia kusitisha ilipofikia hatua ya Usajili mwaka 2017 na hatimaye kuja kuanza tena mwaka jana 2021, pia Mwenyekiti alielezea Dhumuni la kuanzishwa kwa Wachagawote ambapo alitaja ni Umoja huo utajikita kumnufaisha Mwanachama wake kwenye maswala makuu mawili nayo ni Kijamii na Kiuchumi.
TAARIFA FUPI JUU YA KIKAO KILICHOPITA
Mwenyekiti pamoja na Katibu walitoa taarifa fupi juu ya kikao kilichopita kuhusu mahudhurio, maazimio Pamoja na michango ya Mawazo ya wajumbe. Ambapo kikao kilichopita kiliazimia kwa kuipitia Rasimu ya katiba pendekezwa na kujiridhisha kama iko sahihi na kufatilia usajili wa Umoja Wachagawote.
UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA KIKAO KILICHOPITA
Kikao kilichopita tuliazimia kufutilia taarifa juu ya usajili wa Umoja wa Wachagawote na Mwenyekiti na Katibu walifuatilia kuhusu usajili pale Wizara ya mambo ya ndani na taarifa za awali zilipatikana na kulikuwa na mambo muhimu 9 ya kuzingatia ili kufanikisha Usajili;
Katiba ya kikundi na kanunii
Ada ya maombi
Ada ya uandikishaji
Ada ya mwaka
Taarifa ya mkutano uliopitisha katiba
Orodha ya wanachama waasisi wasiopungua 10
Wasifu wa viongozi wa chama na picha zao
Barua ya kuungwa mkono kutoka mamlaka inayohusika
Barua ya maombi kutoka Wachagawote wenyewe, Pamoja na fomu.
Mwenyekiti alizungumzia kuhusu swala la katiba na katiba aliyojadiliwa na kupendekezwa ilikuwepo ili kuona kama kuna marekebisho yanayohitajika kabla ya kwenda kwa mwanasheria kuhakikiwa .
Pia Katibu alitoa ufafanuzi juu ya garama za usajili Pamoja na mahitaji ya msingi kwa ajili ya usajili.
Kama ifuatavyo
Katiba kuhahikikiwa na kupangwa na mwanasheria = 50,000=
Garama za maombi ya usajili = 50,000=
Garama za kuandikisha = 100,000=
Ada ya mwaka = 50, 000=
Garama ya sanduku la posta = 58,000=
Usafiri kwenda Dodoma = 160,000=
Jumla 468,000=
Mwl.Thadey aliendelea kufafanua kuwa gharama hizi za usajili Pamoja na gharama nyingine za kuendesha Umoja huo zitatolewa na wanachama hai kwa kutoa Kiingilio na Ada za kila mwezi au Harambee pale itakapolazimika kufanya hivyo kwa maslahi ya Umoja huo na wakiongozwa na Katiba.
Wajumbe walipata nafasi ya kutoa maoni na ushauri wao ili kufanikisha malengo ya Umoja wa Wachagawote.
Pamoja na michango mingine ya mawazo iliyotolewa na wajumbe, kikao hicho kilipendekeza kuwa taarifa itolewe kwa yeyote ambaye ni MCHAGA na ikiwa kuna Mchaga mwenye nia ya kujiunga anataka kujunga na Kuwa Mwanachama hai wa Wachagawote anapaswa kuijua historia ya Umoja wa Wachagawote na kufahamu malengo na akubali kuheshimu utaratibu na pia awe tayari kulipa kiingilio pamoja na ada zote za kila mwezi kuanzia April 2022 hadi mwezi ule aliojiunga rasmi.
Ifahamike kuwa kwa sasa unaweza kuwa mwanachama hai kwa kutoa Kiingilio na Ada ya kila mwezi;
Kiingilio 50,000=
Ada ya mwezi 20,000=
Kumbuka kuwa kiwango hiki kinaweza kutolewa kwa awamu ndani ya mwezi mmoja mwanachama uwe umemaliza kulipa garama za uanachama. Pia kikao kilipendekeza Mchaga yeyote anayehitaji kuwa mwanachama ni lazima amalize malipo ya Kiingilio na Ada ya ndani ya mwezi mmoja Pia kikao kilipendekeza kiingilio cha uanachama kiwe kinabadilika kutokana thamani husika na hali ya maisha halisi.
Kikao pia kilipendekeza kuwa ili kuweka usawa aliyejisajili mwaka huu akatoa kiingilio isiwe ananufaika sawasawa na atakayekuja kujisajili mwakani. Hiyo ikiwa na maana ya kwamba wakati wa Mafao, ni vyema Umoja wa Wachagawote ukawa unawapa kipaumele wale Wanachama walioanza tokea Mwanzo.
MENGINEO
Mjumbe mwingine alishauri kuwepo na sehemu ya kuhifadhi fedha za wanakikundi ili ziwe salama na zisikae kwenye mikono ya watu hivyo Mwenyekiti alifungua akaunti ya M-KOBA ambayo ni 1167955 siku hiyo hiyo na wanachama waliokuwepo wakaungwa..
Pia kikao kilishauriwa tuwe na line ya voda kwa kipindi hiki cha mpito kwa ajili ya M-KOBA ilikuweza kufanya miamala Pamoja na mambo mengine, tofauti na mitandao mimgine huwezi kupata menyu ya M-KOBA kwenye line za mitandao mingine ila unaweza kulipa kwa kitumia mitandao mengine.
Mjumbe mwingine alishauri tuanze kuchangia garama za mwanasheria kwa ajili ya kurekebisha katiba kwani ni ya muhimu Zaidi mana bila hiyo hatuwezi kufanya chochote. Na michango ilitolewa na wajumbe kama ifuatavyo;
PIUS KIWANGO 50,000=
RIZIKIEL MMARI 10,000=
INNOCENT MUSHI 10,000=
AVELINI MUSHI 10,000=
_______
JUMLA 80, 000=
Ambapo kiasi cha shilingi elfu 50 kama malipo ya mwanasheria kwa ajili ya kurekebisha katiba ikae katika muundo unaotakiwa kwenye Usajili.
Kikao kilifungwa na mwenyekiti mnasaa 2 kamili usiku
