Ni kikao cha nne cha Wachagawote
Kama ilivyo utaratibu wao wa kukutana kwa lengo kujadiliana namna ya kukuza kikundi chao kinachotambulika kama UMOJA WA WACHAGAWOTE na awamu hii kilifanyika tarehe 10 April 2022 na eneo walipokutana ni pale pale LEGO HOTEL-Shekilango Sinza Dar es Salaam muda wa kuanzia saa 11 jioni hadi saa 1 jioni.
Kikao hicho cha Wachagawote kilichoitishwa na Mwenyekiti na Muasisi wake Ndg. Rizikiel Mmari, kama ilivyo utaratibu wao kujiwekea Agenda za kikao, hivyo kilikuwa na Agenda zipatazo saba; 1. Kufungua kikao 2. Mahudhurio 3. Utambulisho 4. Taarifa fupi za kikao Kilichopita 5. Uhamasishaji 6. Mengineyo 7. Kuahirisha kikao.
Kikao kilifunguliwa mnamo saa 11 jioni na Mwenyekiti Ndg. MMARI kwa kuongozwa na sala iliyofanywa na Mjumbe na Mwanachama Dada Rose Mallya.
Kikao kilipata bahati ya kuhudhuriwa na wajumbe sita ambapo walipata nafasi ya kila mmoja kujitambulisha Makazi anayotoka, Kazi/Biashara anayofanya, hali ya Ndoa/Mahusiano aliyonayo pamoja na Majina kamili kama majina yao yanovyoonekana hapo chini;
1. RIZIKIEL A. MMARI
2. RIZIKI F. MSAKI
3. THADEY F. KITALY
4. ROSE MALLYA
5. INNOCENT MUSHI
6. ALOYCE F. SOKA.
Baada ya kujitambulisha kwa Wajumbe wote, Mwenyekiti Ndg. Mmari aliwakaribisha wageni ambao ndio ilikuwa mara yao ya kwanza kuhudhuria vikao vya Wachagawote, kisha alitoa taarifa fupi kwa wageni kufahamu historia ya Umoja wa Wachagawote na pia yeye kama Muasisi wake alieleza kwa ufupi dhumuni na lengo la kuanzisha Umoja wa Wachagawote.
Pia Mwenyekiti alitoa taarifa juu ya utekelezaji wa maazimio ya mwezi April 2022 yaliowekwa ya kikao kilichopita, huku akitumia muda ule kutolea ufafanuzi lile wazo alilolileta kwenye kikao kilichopita Umoja wa Wachagawote kuwa na chombo cha Habari cha kidigiti ambacho pamoja na kuwa na lengo la kutumika kama sehemu rasmi ya kutoa taarifa za Umoja au kuzungumza na Dunia, pia chombo hicho anatarajia kutumika kama chanzo cha mapato ya Umoja kwa sababu ya lazi itakayokuwa inafanya ya kutoa taarifa au elimu kwa wafatiliaji wake hivyo kualika wafanya biashara na makampuni kuweka matangazo yao.
Akiendelea na ufafanuzi Ndug. Mmari alisema chombo hicho cha habari licha ya kuwa kitamilikiwa na Umoja wa Wachagawote hakitokuwa na mipaka yoyote kuhusiana na maudhui yake au aina ya habari zitakazoyolewa nacho kwani kitakuwa chombochombokama vilivyo vyombo vingine vya habari vy kibiashara.
Ndg. Mmari pia aliendelea kusema kuwa kwenye upande wa matangazo kutakuwa na kipaumbele kwa wanachama kwa kupewa ofa ya kutangaza biashara zao bure au nusu ya bei kwa nia ya kumnufaisha Mwanaumoja mwenye nia ya kuweka Tangazo lake.
Katika kikao hicho Katibu wa Umoja wa Wachagawote Mwl. THADEY KITALY alitoa ufafanuzi kuusiana na maazimio yaliowekwa ya kikao kilichopita na baadhi ya hatua zilizofikiwa na baadhi utekelezaji uliofanyika.
Mh. Katibu pia aliiendelea kusema kuwa kikao kilichopita kiliazimia kila mwanachama ajitahidi kwa mwezi April 2020 awe amemaliza kutoa fedha Tshs 70,000/= ikiwa na mchanganuo wa Tshs. 50,000 ni ya Kiingilio cha kuwa Mwanachama wa Umoja wa Wachagawote, na Tshs. 20,000/= ni Ada ya Uanachama kwa mwezi huo wa April 2022 ambapo kwa matarajio ni kupata jumla ya Tshs 700,000/= kwa wanachama wote 10 kama kila mmoja atatoa Tshs. 70,000/= iliyokusudiwa na kikao hicho.
Pia Mh. katibu aliendelea kuelezea kuwa wajumbe walishauri iruhusiwe kwa Mwanaumoja kutoa fedha hizo kwa awamu ili kuwawezesha wale ambao hawana uwezo wa kutoa fedha hizo kwa mkupuo mmoja ijapokuwa mbeleyetu tuna mahitaji ambayo tunahitaji pesa za haraka kutimiza mahitaji kama vile kulipia gharama za Mwanasheria anayerekebisha na kuipangilia Katiba pamoja na gharama za Usajili wa Kikundi.
Wajumbe kwenye kikao kile walianza kutoa fedha za Uanachama ambapo pale pale kwenye kikao kilipatikana kiasi cha Tshs. 80,000/= ambayo Tshs. 50,000/= alikabidhiwa Mwl. Thadey Kitaly (Katibu) kwa ajili ya kumlimpa mwanasheria atakayeirekebisha na kuipangila vyema katiba Pendekezwa ya Umoja wa Wachagawote na kile kiasi cha Tshs. 30,000/= kilichobakia kilihifadhiwa kwenye akaunti ya Wachagawote iliyofunguliwa kidigiti kwa mtandao wa Vodacom Tanzania kupitia M-PESA huduma za vikundi inayofahamika kama M-KOBA ambapo kuanzia siku ile ya kikao tarehe 03 April 2022 ndio ikaanzishwa rasmi Akaunti ya Wachagawote kupitia mtandao wa Vodacom Tanzania.
Katika kikao hicho cha nne cha Umoja wa Wachagawote Mwenyekiti Ndg. Mmari alisema wajumbe wote tunahitaji kufanya uhamasishaji kupitia magroup ya whatsapp ya Wachagawote kuhusu Umuhimu wa kutoa Kiingilio na Ada ya Uanachama ya kila mwezi ili Umoja wa Wachagawote uweze kijiendesha.
Akiendelea kusema Ndg. Mmari alisema ili kufanikisha malengo ya Wachagawote kuwa na Miradi kama inavyotarajiwa, itahitajika fedha na zaidi tunahitaji kuwa na Wanachama wengi zaidi ili kwa pamoja tukishirikiana tunakuwa na mchango mkubwa jambo litakalotuwezedha kwa wingi wetu iwe rahisi kupata huduma muhimu kwa gharama ndogo au bure kabisa kwa sababu tutahudumiwa kama kundi kubwa, hivyo ni muhimu wajumbe waelewe kwanini tunatoa kiingilio na ada ya mwezi ili wajivunie kutoa kwa nia ya kufanikisha malengo ya Umoja huo.
Pia Mwenyekiti alishauri wajumbe kuwaeleza watumiaji wa magroup ya whatsapp nini faida za kuwa Mwanachama wa Wachagawote na nini faida ya sisi wote kuungana na kuwa kitu kimoja kwa kujihakikishia kupata bima ya afya, huduma za kisheria, ushauri na malezi ya kibiashara na mafao mbalimbali ya kijamii, mikopo ya nyumba au mitaji ya biashara n.k.
Katika kikao hicho Wajumbe walipata nafasi ya kuuliza maswali na pia kutoa maoni yao ambapo Dada RIZIKI MSAKI yeye alipenda kupewa ufafanuzi kuhusu Mwanaumoja ananufaika vipi kwenye Mafao ya kifo wakati anapopatwa na msiba wa kuondokewa na mpendwa wake kama inavyoeleza Katiba.
Katika kikao hicho kulikuwa na mengineyo ambapo kutokana na watumiaji wengi wa magroup ya whatsapp kushauri link isitishwe kwa sasa ili kuepusha watumiaji wengi ambao sio wachaga kuingia kwenye magroup hayo Wachagawote01 na Wachagawote02, wajumbe walipendekeza link ya group la wachagawote ibakie ili tupate wanachama wengi kwakuwa ni moja ya lengo la kuwapata wanachama wengi kupitia mitandao ya kijamii.
Kutokana na ile kadhia wanayoipata viongozi wa magroup ya Wachagawote kutoka kwa watumiaji wachache wenye tabia ya kuvunja sheria za group na kuwa kero kwa wengine, Mjumbe Dada yetu Rose Mallya alishauri tuwavumilie kwa namna yoyote ili lengo la kuwa na wanachama wa kutosha lifikie. akaendelea kushauri Dada Rose kuwa hao wachache wakivumiliwa labda watabadilika na kuwa msaada mkubwa kwenye Umoja wa Wachagawote kama watapewa muda kujirekebisha, akasisitiza kuwa, mara nyingi kila wakutanapo watu wa marika/elimu tofauti ni lazima kuwe na kupishana kwenye mitazamo na uelewa... Jambo la muhimu ni kupeana nafasi kwa kila mmoja kwani tunaamini kila mmoja anayo sehemu ya kugeuka kuwa msaada kati yetu.
Akiendelea kutumia nafasi hiyo ya kutoa maoni yake Dada Rose pia alitoa ushauri kuhusiana na makatazo yaliyowekwa kwenye magroup kwa watumiaji kutotangaza Biashara zao alipendekeza Biashara ziruhusiwe japo kwa siku moja kwa wiki kwa mfano JUMAMOSI au JUMAPILI iwe kila mtumiaji mwenye biashara au tangazo la kazi wanazofanya wanaweza kutuma kwenye magruop ya Wachagawote na iwe kwa utaratibu wakutuma angalau picha zisizidi tano kwa kila mtumiaji mwenye matangazo. Kwa pamoja wajumbe wote kwenye kikao walimuunga mkono dada Rose kwa kupitisha kwenye kikao iwe ruksa kutuma matangazo ya kibiashara kwa watumiaji wa magroup ya Wachagawote ili kupata wateja kwa muda huu mpaka utaratibu mwingine utakapotolewa.
Pia kwa kuongezea Mwenyekiti Ndg. Mmari alifafanua kuwa mpango wa Umoja wa Wachagawote ni kuwasaidia Wanachama wake wanaofanya biashara kuzitangaza biashara/huduma wanazozifanya kuwafikia wateja wengi.
Kulithibitisha hilo, alionyesha mfano wa tovuti ya habari itayowawezesha wanaumoja kuweka matangazo ya biashara zao ili kuwafikia wafatiliaji wengi zaidi na kupata wateja wengi wa uhakika.
Hatimaye kwenye kikao hicho Wajumbe walikubaliana kuwaelemisha wengine yale tuliyojadili na kufahamishana kuhusu hatua za kukuza na kuimarisha Umoja wa Wachagawote na faida za kuwa Mwanaumoja.
Mwishowe Kikao kilifungwa mnamo saa 1 Jioni kwa Mwenyekiti Ndg. Mmari kuwashukuru wajumbe wote kwa kuwepo kwao Pamoja na michango yote waliochangia kwa ajili ya ustawi wa kikundi cha Umoja wa Wachagawote pamoja na magroup yake ya whatsapp.
Baadhi ya Picha za Wajumbe waliohudhuria kikao cha 4(b) cha Umoja wa Wachagawote
![]() |
| Rizikiel Mmari |
![]() |
| Mwl. Thadey Kitaly |
![]() |
| Innocent Mushi |
![]() |
| Riziki Msaki |
![]() |
| Rose Mallya |





