Wachagawote: ''...Kupost Matangazo Kwenye Group Ruksa...''


 

''... yaani kila inapofika Jumamosi na Jumapili kwenye magroup ya Wachagawote unaruhusiwa kutuma picha za vitu unavyouza au matangazo ya nafasi za kazi... kwahiyo tunaruhusu utume picha angalau tano tu usizidishe ili kuruhusu pia na wenzako wapate nafasi ya kuonyesha picha za biashara zao...'' 

Hayo yamesemwa na Admin Mkuu wa magroup ya Wachagawote Ndg. Rizikiel Mmari, kwa njia ya simu  baada ya kuulizwa na mwandishi wetu kuhusiana na mapendekezo yaliyotolewa na Wajumbe kwenye kikao cha nne(b) ambapo walipendekeza kuruhusiwa Watumiaji wa magroup hayo kuweka matangazo ya biashara zao kwa mfumo wa picha jambo ambalo hapo awali lilipigwa marufuku na kufikia kutungiwa sheria rasmi zinazoendesha magroup hayo.  

Akiendelea kusema hayo Mwenyekiti Ndg. Rizikiel Mmari ambaye pia ndio Muasisi wa Kikundi hicho cha Kijamii kinachojulikana kama Umoja wa Wachagawote(U.WA.WO.) alisema wao kama viongozi wameona ni vyema kuwasikiliza wanagroup wanachotaka kwa kuwapa ruhusa waweke matangazo ya biashara kama walivyopendekeza kwenye kikao cha nne(b) kilichofanyika tarehe 10 April 2022.

Hapo awali kuliwekwa makatazo kwa wanagroup kutokutuma picha za biashara kwenye group kutokana na sheria za group kukataza.
Magroup hayo Wachagawote yalianzishwa maalumu na Ndg. Mmari kwa nia ya kupata taarifa na pia kutumika kama njia mojawapo ya kuwasiliana na Wanachama wa Umoja wa Wachagawote kwa urahisi kupitia Mtandao wa kijamii wa Whatsapp.

Hivyo basi kwa ruhusa hiyo wanagroup wanayo nafasi ya kuwatangazia wanagrouop wenzao shughuli au biashara wanazozifanya kwa kutuma picha au link za kibiashara japo picha tano kwa mtumaji mmoja.

Hata hivyo kilichoruhusiwa ni matangazo ya biashara pekeyake na kuyafanya makatazo mengine yaendelee kusalia vile vile.

Kama bado ujajiunga na Magroup hayo Bofya kuingia Wachagawote01 na Wachagawote02 


Je, una maoni gani?

Newer Post Older Post