MABORESHO YA DAFTARI LA MWANACHAMA HAI



"... kiukweli inabidi tuliboreshe Daftari ya usajili na hatua za kimaendeleo tunaanza na Wanachama hai 20 tu walio tayari kuungana nasi..." Haya yalisemwa na Ndg. Rizikiel Mmari (Mwenyekiti/Muasisi wa Umoja wa Wachagawote) alipokuwa anaongea na mwandishi wetu leo mchana. 

Umoja wa Wachagawote unalazimika kuchukua maamuzi magumu kwa kuwapa kipaumbele wafatiliaji wake ambao watakuwa tayari kwa Kujisajili na kuwa wanachama hai wa Umoja wa Wachagawote.

Ifahamike kuwa ni mwanachama hai ndio mnufaika sahihi wa mafao yote yanayotolewa na Umoja huo. 

Mwenyekiti Mmari alisema.. "Kwa kuwa malengo ni kutoa mafao kwa walengwa, ni wazi uongozi wa Umoja unapaswa kusimamia mchakato wa kuwapata walengwa sahihi na kuhakikisha utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Katiba unafatwa na kila mwanachama hai anatimiza masharti ya Umoja na hali kadhalika Chama nacho kimpatie yale mafao yake bila ukakasi wa aina yoyote ile..."

Akiendelea kueleza Mmari alisema "... Umoja wa Wachagawote unaazimia kuwa na Miradi yake na faida za miradi hiyo zitakwenda moja kwa moja kwa wanachama wenyewe kwakuwa wao ndio walioweka jasho lao kuutunisha mfuko wa Umoja..."

Akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu mpango hiyo Mmari alisema, "... kumekuwa na mtazamo hasi kwa wafatiliaji wetu kwenye magroup ya Wachagawote WhatsApp na pia kwenye kurasa za Facebook na Instagram kuwa Wachagawote ni kama hakuna jambo lolote linaloendelea ili kuonyesha namna ya dhamira husika ya kuanzishwa kwa Umoja wa Wachagawote na hivyo kuwafanya wafatiliaji kukata tamaa na wengine kujiondosha kwenye magroup ya WhatsApp kwa kile wanachokiona ni kupotezewa muda..."

Mmari aliweka wazi, "...naomba ifahamike kuwa ili kufanikisha mipango hii ya Umoja wa Wachagawote ni lazima tuwe na watu makini wenye maono chanya na wanaoweza kukubali kujitolea kuujenga Umoja huu kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo. Na ikumbukwe kuwa sio lazima tuanze na watu wengi kwa hapa mwanzoni... sana sana tunahitaji watu 20 tu na kama watazidi basi ni 50 tu, na wengine watajiunga nasi hapo badae baada ya kuona hatua tulizopiga."

Hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Umoja wa Wachagawote ni kuwa kuanzia sasa kutakuwa na daftari maalumu la kuwaandikisha Wachaga 20 hadi 50 tu ambao ndio watakaoanza kujenga misingi ya Umoja huu. 

Wachaga hao 20 hadi 50 watalazimika kuwa wanachama hai (watalipa kiingilio 50,000 na ada za kila mwezi 20,000) na kuhakikisha wanahudhuria vikao vyote na kushiriki uanzishwaji wa miradi ya Umoja wa Wachagawote.

Kwa mwanzoni watakuwa na malengo ya miezi 3 halafu itafata na malengo ya miezi mingine 5 kisha malengo mafupi ya miezi 3 na baada ya hapo ndio wataanza kuruhusiwa wanachama wengine kuingia kwenye malengo ya mwaka mmoja na baada ya huo mwaka wataingia malengo ya miaka miwili miwili kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo na kufanya kutimia kwa Awamu ya kwanza ya miradi ya maendeleo. 

Baada ya hapo utaanza Awamu ya pili ambayo ni uwekezaji mkubwa wa kila Mkoa kwa kuchukua aina ya miradi kulingana na mkoa husika.

Mmari anazidi kuelekeza kuwa, "...wanachama hai watakuwa na mifumo maalumu ya mawasiliano ya Umoja na hata group la WhatsApp litakuwa na matumizi husika tu na sio vinginevyo na kama mwanachama atakiuka atawajibishwa kwa faini... pia ada za kila mwezi zitapaswa kulipwa kwa wakati na kama ikicheleweshwa itatozwa faini..."

Mmari alisema wameamua kufanya hivyo ili kufikia malengo ya Umoja wa Wachagawote ndani ya muda uliowekwa, kwa kuwa yanayoendelea hivi sasa hayawezi kuwafikisha kwenye safari ya mafanikio ya Umoja wa Wachagawote.

Kwa sasahivi kama yupo Mchaga yeyote anayejiona yupo tayari kujiunga na Umoja anaweza kutuma barua pepe yenye taarifa za utambulisho wako kwenda wachagawote@gmail.com au piga/sms 0659310000















Newer Post Older Post