Kuna Faida Na Hasara Kwa Wachaga Kula Kitimoto

 



Ni kwa muda mrefu sasa Kumekuwepo kwa dhana ya kuwa Kitimoto asili yake ni Uchagani na imkazoeleka kuwa Wachaga wengi wanapenda Kitimoto na wengi ni wao ndio Wafanyabiashara zaidi wa Nyama hii ya Kitimoto, hebu leo nikushirikishe kwa uchache Jinsi Wachaga wamehusishwa na Dhana hiyo na pia tutaangalia pia Faida na Hasara za Ulaji wa Kitimoto.

Wachaga na Asili ya Kitimoto

Pamoja na kilimo cha mazao, Wachaga hupendelea sana kufuga wanyama mbalimbali hata nguruwe.
Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la “Kitimoto” ni moja ya mambo yaliyoenezwa na wachaga.
Ulaji wa “kiti moto” haukupendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo wachaga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu.



Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo waisalmu kwao kula nguruwe ilikuwa “ruksa”.
Hivi leo imebadilika sana kwani karibu kila konanya jiji la Dar es Salaam huduma ya kitimoto haikosekani na zaidi inasemekana upikwaji wake sehemu zingine hazijafikia umahiri wa mapishi ya jiji la Dar es Salaam,
imegundulika kuwa wapishi wengi wa kitimoto kwa jiji la Dar es Salaam ni Wachaga na wamekuwa wakibuni aina mbalimbali za vionjo na kuifanya kitimoto inayouzwa maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kuwa na ladha murua kila kukicha na Kitimoto Kupendwa zaidi, pia kuwafanya Waandaaji watambulike zaidi kutokana na umahiri wa mapishi ya Kitimoto na kumepelekea sehemu inayouzwa kitimoto na ikawa Mpishi wake ni Mchaga basi eneo hilo hupendwa zaidi na walaji wa Kitimoto.

Kitaalamu kuna Faida kadhaa unapokula Kitimoto: 

1. Ina vitamin muhimu katika mwili wa binadamu; ambazo ni B1, B6 and B12
2. Ina madini ya chuma ambayo husaidia kuimarisha mifupa.
3. Inaimarisha ngozi yako na kuifanya iwe laini.
4. Ina madini ya magnesium kwa wingi yenye faida kwa binadamu.
5. Ina protein ya kutosha inayosaidia ulinzi wa mwili.
6. Ina mafuta yanayotoa nguvu mwilini.

Hatahivyo yapo Madhara kadhaa yatokanayo na kula Kitimoto:

Licha ya faida zilizotajwa hapo juu, pia kuna hasara ya kutumia nyama hii ambayo ina sumu ya carcinogen inayosababisha kansa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani ( WHO) na The International Agency for Research on Cancer!! utafiti  unaonyesha kuwa ukila nyama hiyo kila siku gramu 50  uwezekano kupata kansa unaongezeka kwa asilimia 18.
Pia inasababisha homa iitwayo Swine Flu kwa binadamu ambayo inatokana na virusi vinavyosababisha mafua kwa binaadamu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyiwa na Centers for Disease Control and Prevention inaonyesha virusi vya Influenza  H1N1 na H3N2 vinavyotokana na kiti moto, kusababisha maradhi ya mlipuko kwa nchi za bara la Amerika.

Vilevile, nyama ya nguruwe ina minyoo wajulikanao kwa jina la trichinella worm  ambao ni vigumu kufa kwa joto hata la Centigrade 100.

Utafiti uliofanyiwa na WHO mwaka 1988, ulionyesha kitimoto  iliyopiwa kwa joto la C. 104,  asilimia  52.37  ya trichinella worm huwa wanabaki hai.

Wadudu hao wakiingia  mwilini mwa binadamu husababisha ugonjwa ujulikanao kwa jina la trichinosis; ambao huwa na dalili zifuatazo:

(i) Homa kali
(ii) Kichwa kuuma
(iii) Kukosa nguvu
(iv) Maumivu ya nyama za mwili
(v) Macho kuwa rangi ya pink (conjunctivitis)
(vi) Kuvimba uso na kope
(vii) Kudhurika  na mwanga
(viii) Kitimoto ina virus aina ya Hepatitis E virus (HEV) ambaye husababisha homa ya ini aina E

Wadudu wengine wanaopatikana katika kitimoto ni:

(i)  Virusi vya Nipah virus
(ii) Menangle virus
(iii) Viruses katika  kundi la Paramyxoviridae
Wote hao huwa wana madhara kwa binadamu

Nyama ya nguruwe husababisha maradhi yanayokianza na madawa yenye kupambana na vimeleo vya magonjwa, yaani ‘Antibiotics’ na kwa mujibu wa WHO nyama ya hiyo pia ina minyoo aina ya Taenia solium.
Minyoo hii hutokana kutopikwa vizuri nyama hiyo.  Minyoo hii ikiingia mwili wa binadamu husababisha matatizo ya mfumo wa fahamu (central nervous system) iitwayo neurocysticercosis, na kusabisha kifafa.
Asimilia 3 ya wagonjwa wenye kifafa huwa ni wale ambao hushambuliwa na minyoo hii ipatikanayo kwenye nguruwe.
Watu milioni 50 duniani wanaopata kifafa  huwa ni walaji wazuri wa nguruwe.




#Nambie Mchaga mwenzangu, wewe umejifunza Faida na Hasara za ulaji wa Kitimoto?
# Je, wewe unapendelea kula wapi Kitimoto?
# Mimi ntafurahi sana Mchaga mwenzangu ukinialika popote ulipo nikaungana nawewe tule kitimoto pamoja.
# Niandikie ujumbe wako hapo chini ungana namimi tuendelee kuukomaza undugu wetu daima

Newer Post Older Post