Ni kweli tunaogopa Matapeli, lakini ni muhimu wa kuambiana Ukweli pia.

 



Mimi Mmari ninakuandikia... 

Kwa hali ilipofikia hivi sasa kila mtu anajichukulia yeye ndio anastahili kupata na mwingine ndio anapaswa kukosa, 

Swali litazaliwa hapo; 

Je, nani atafanikiwa kuwa wa kukosa ili hali kila mmoja anajiona yeye ndio wa kupata?

Jibu sahihi; Tunalazimika kuachana na ubinafsi na tuungane kusimamia haki ya kila mmoja pasipo ubaguzi na kumuona kila mmoja wetu anastahili kupewa sawa sawa na vile tunavyostahili kupewa sisi kwa sisi.

Kwa upande wangu, namshukuru Mungu nimepata hichi kibali cha kuwaunganisha Wachaga kupitia mitandao hii ya kijamii, imekuwa bahati kwangu kukutana na wewe hapa na sio kwamba mimi ni bora sana, au mimi naweza zaidi yako, ninachokifanya hata wewe unaweza kufanya na yawezekana ukawa wewe ni bora zaidi yangu.

Kwa aina ya mfumo ninaotumia(Mitandao ya kijamii) ni eneo ambalo limekumbwa na shambulio la kiuvamizi wa mitazamo hasi zaidi na kupelekea kuchukuliwa kama ni mifumo isiyoweza kukubalika kwa maana ya kupewa kipaumbele na hasa kuaminika.

Wazo langu la kuanzisha Umoja wa Wachagawote limepokelewa vyema mioyoni mwa Wachaga wengi kwa zaidi ya 100% 

Isipokuwa pamoja na kupokelewa hivyo lakini bado ninalo deni mioyoni mwa Wafuasi wengi wanaofatilia kuhusu Wachagawote, deni hilo ni KUAMINIKA.

Swala la kuaminika kwa kiasi kikubwa linahitaji mhusika kufahamu uhalisia wa maisha yetu na pia mifumo tunayotumia ili kufikia hiyo hali ya kuaminika. 

Ninatambua kuwa wengi wetu wamepitia kukutwa na matukio mbalimbali ya kutapeliwa na hata na watu wa karibu kabisa na matukio mengine yanafanana kwa  namna moja ama nyingine.

Hata hivyo tutakubaliana kuwa sio kila anayekuja kwa njia hiyo basi nayeye ni tapeli au mwizi wa mtandaoni kama waliokudhuru hapo awali. 

Kumbuka kuwa hata wewe ungefanya ninachokifanya mimi sasahivi, pia usingeaminika na pia ungehisiwa kuwa tapeli kama ninavyochukuliwa mimi hivi sasa.


Sasa hapa hebu nikuandikie machache ya kutafakari...

1. Kama njia ya mitandao ya kijamii inatafsiriwa kuwa ndio ya kitapeli, unafikiri tutumie njia ipi?

2. Kwa hali tuliyofikia ni lazima tuungane ili mambo yasonge, na hata kama nisingekuwa mimi basi angekuwepo mwingine au wewe ungekuwa ndio Mmari.

3. Kama haupo tayari kuweka Imani yako kwenye hili haimaanishi ni lazima kwako kuamini, kuna mafanikio mengi umeyapata bila ya sisi kuamini unachokifanya, hali kadhalika tunaweza kufika pasipo lazima ya kuaminiwa na wewe.

Kwakuwa wewe ni Mchaga mwenzangu napenda kukujulisha kuwa mimi na wewe tunapasa kuambiana UKWELI hata kama unaumiza nyoyo zetu.

Siku moja ina masaa 24, jitahidi kutumia angalau masaa 2 tu kwa siku kutafakari ni kwa kiasi gani umejiandaa kujitolea kwa ajili ya Wachaga wenzako waliopo pale Kijijini kwako ambao kila unapoenda wanakuuliza umeniletea nini na ukiondoka wanakuuliza unatuacha acha aje.


Nimetangulia kuandika hapo juu kuwa ni vyema tukaambiana UKWELI hata kama unaumiza, naanza mimi halafu wewe utaendelea... 


UKWELI wa Mkuu au Ukweli Mtakatifu  ni kuwa hakuna mtindo maisha ulio mtamu na mzuri zaidi ya ule mtindo wa kuishi ukiwa unamiliki KIPATO cha UHAKIKA yaani hata kama ni elfu 5 tu unaipata kwa siku na ukawa na uhakika kuwa utaendelea kuipata kila siku hiyo elfu 5 hadi uingie kaburini. Hayo ndio matamanio ya watafutaji wengi wanatamani kujiweka kwenye mtindo huo wa maisha... yaani jua likizama tu unauhakika elfu 5 yako imetumbukia kwenye akaunti, na hapa nimeitolea mfano elfu 5 tu japokuwa yawezekana ukawa una uhakika wa kupata zaidi ya hapo kwa maisha yako yoote. 

UKWELI mwingine Mtakatifu ni kuwa hakuna njia nyepesi zaidi kufanikisha kuwa na hicho kipato cha uhakika zaidi ya  kujiunga na vikundi vya kusaidiana vilivyoundwa kwa mfumo wa kibiashara au uzalishaji wa fedha.

Kwa eneo hili la vikundi vya kusaidiana, unaweza usielewe au yawezekana ukaelewa tofauti na malengo husika. Kwa ufupi naweza kukupa ufafanuzi ili usibakie gizani kama ulikuwa hujui ni kuwa vikundi vya kusaidiana vipo vya aina nyingi sana kwa kijinadi lakini vyote vinasimamia mifumo mmoja tu nao ni  BIASHARA. Kwa mfano vikundi maarufu ambavyo kila mmoja wetu anavifahamu hata wewe waweza kuvisemea ni hivi vikundi vinavyotambulika kama KANISA na MSIKITI,  hivi ni vikundi vya kusaidiana kukuza Imani zetu na pia kukuza soko la Amani na Nidhamu (Kwa atakayenitafsiri tofauti naomba anisamehe kwa sababu sitaweza kulazimisha unielewe, na atakayenielewa naomba ukawaeleweshe na wengine) na kwa sababu ya kulinda Imani zetu naomba nisifumue sana hayo maeneo ya kiimani sana sana nitaishia kwenye biashara inavyoingia japokuwa sio rahisi wewe muumini kuitambua na hata kama utaitambua wala haina madhara zaidi inafaida kwako na wengine pia.

Iko hivi, kama wewe ni mfanyabiashara na unataka kufanikiwa kibiashara ni lazima utumie mifumo ya kupata hayo mafanikio, mfano ili ufanikiwe kuuza bidhaa yako  kwa wateja wengi inakupasa uwe umeshusha bei na uhakikishe  umewafikia wengi zaidi ili kati yao wawe wamenunua kwa wingi. Na ili uweze kulifikia hilo itakubidi uwekeze sana kwenye matangazo na uwe na bajeti ya kutosha kutangaza hiyo bidhaa yako kama makampuni makubwa wao wanatumia 60% ya mapato yao kujitangaza kila siku pasipo kukoma yaani maisha yao yote wanawekeza kwenye kujitangaza ili kuwafikia wateja wengi na hasa hasa kujenga familia za kibiashara. 

Kwa hiyo ukiwa na kanisa au msikiti hauhitaji kuwekeza pesa nyingi kwenye kujitangaza kibiashara sana sana utawekeza nguvu nyingi kuhubiri Imani husika na utatengeneza familia ya kibiashara ambayo kwa upande wa kidini inaitwa WAUMINI kama ilivyo kwenye michezo wanaitwa MASHABIKI ambao inapokuja swala la kuuza bidhaa hauhitaji kuwashawishi kwa matangazo sana sana ni kuwaelekeza tu kwa kuwapa taarifa na wao watanunua tu bidhaa yako haswa haswa ikiwa ni bidhaa inayoendana na mahitaji yao muhimu na hapo ndio mafanikio yanapoonekana kama unavyoona mashule yanayomilikiwa na Kanisa au msikiti huwa hayakosi wanafunzi wa kusoma au miradi yoyote inayofanywa na Kanisa na Msikiti au inayofanywa na hizi timu za Simba na Yanga huwa miradi hiyo inafanikiwa kwa 100%.

Hivyo basi UKWELI muhimu hapa unaopaswa kuambiana ni kuwa mimi na wewe ni lazima tuungane kuhakikisha tunaujenga UMOJA WA WACHAGAWOTE ili utufikishe kwenye mafanikio ya kibiashara na kuwa msaada wa vizazi vyetu haswa kiuchumi kwa kuwa kupitia Umoja huu tutafanya jambo lolote kwa kuwa tutakuwa tumewaunganisha Wachaga wote ambao inakadiriwa tumefikia Milioni 21.62 duniani kote(labda namba yaweza kubadilika baada ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi)

Sasa UKWELI usiofichika ni kuwa kati ya hao Wachaga zaidi milioni 21 tukafanikiwa kuwa na Wanachama hai milioni 1 pekee sawa na 5% ya Wachaga wote duniani inatuwezesha sisi wanachama hai kulelewa na hao wengine ambao sio wanachama hai kwa kuwapatia huduma muhimu kama makanisa na misikiti inavyofanya ambapo kwetu ndio bidhaa tutakazouza kwao na sisi kujipatia mafaniki, na inawezekana ukashtuka sasahivi baada ya kusoma hapa na mimi sitakushangaa kwa kushtuka kwako nakukumbusha tu hapa tunaambiana UKWELI na kwa kuongezea tu ni kwamba huu mfumo wa kibiashara ndio unaoendesha dunia tukea kuumbwa kwake na sio kwamba haya ninayoandika hapa nimeyagundua mimi tu, huu ndio mpango wa Mungu kwenye kwamba Tupendane na tushirikiane ili kujipatia maendeleo.

Naomba nimalizie kwa kuandika UKWELI unaoumiza kidogo na ukiweza kuelewa utapata Faraja ya milele, 

Hapa duniani ni lazima tuache UBINAFSI na UCHOYO  ili tupate maendeleo kwenye maeneo yoyote yale iwe ni kwenye familia zetu au kazini au hata kwenye makundi yetu mbalimbali.
Kwa kufanya hivyo tutafanikiwa kupata majibu ya milele kwenye maisha yetu na pia kwa ndugu zetu wale pale Moshi wanatuuliza tumewaletea nini na tunaondoka kwa kuwaacha acha je.

Hivyo basi kuungana na kushirikiana haikwepeki kati yetu na ni lazima tuache Uchoyo na Ubinafsi na la kuongezea ni kuwa hata usipojiunga na Umoja huu wa Wachagawote basi hakikisha unajiunga na Kikundi kingine chenye malengo kama haya ya Umoja wa Wachagawote. 


Asanteni kwa kusoma niliyoyaandika mimi Mmari.





Newer Post Older Post