Sisi Wachagawote tunaoishi hapa Dar es Salaam, kwa pamoja tukiwa na familia zetu tutakutana kula Mbuzi choma na Kitimoto vilivyoandaliwa na UMOJA WA WACHAGAWOTE.
Siku ya tukio itakuwa tarehe 30 Mwezi wa 7 Mwaka huu 2022
Eneo tutakalofanyia ni pale Kimara Korogwe jirani na kanisa Katoliki la Kimara Korogwe panajulikana kwa umarufu wa Mbuzi choma na Kitimoto(Kwa Saimon) ni Eneo la wazi mnaoishi maeneo yale mtakuwa mnapafahamu sana na familia nyingi zinapenda kukutana siku ya Jumamosi na Jumapili kula nyama ya mbuzi choma pamoja na Kitimoto.
Jambo letu litakuwa kama ifuatavyo;
Umoja umeandaa chakula na vinywaji maalumu kwa ajili ya siku hiyo na tutaendesha matangazo mtandaoni kuwaalika Wachaga wote wanaopenda kuja kushiriki mlo huo.
Ili tuweze kushiriki tutanunua Vocha maalumu zitakazotuwezesha kula chochote bila kupimiwa(Yaani tutakula hadi tutosheke)
Tutakuwa na Vocha za aina mbili, mojawapo ni ya Tshs 15,000 kwa mtu binafsi na Tshs 35,000 kwa familia yaani Baba, Mama na watoto wawili.
Ukishalipa inakuruhusu kula nyama choma au kitimoto wewe na familia yako kwa kiasi mtakachoweza kumaliza, isipokuwa vinywaji utagharamia kwa idadi na aina ya vinywaji mtakavyopenda kutumia siku hiyo na uzuri ni kuwa bei ya vinywaji tutauziwa kwa bei elekezi(bei ya dukani kwa Mangi)
Muda utakuwa kuanzia saa 7 na nusu mchana hadi saa 12 na nusu jioni na kwa wale watakaopenda kuendelea kukaa kubadilishana mawazo ya hapa na pale tutakuwepo pamoja hadi saa 2 usiku.
Tutakuwa na Wazungumzaji wachache watakaoshirikiana na Mwenyekiti Ndg Mmari kufikisha Ujumbe maalumu kutoka Umoja wa Wachagawote siku hiyo.
Nduguzangu tunawakaribisha sana Wachagawote tuje kula na kunywa pamoja na pia kuzungumza mengi ya Uchagani kwetu.
JINSI YA KUNUNUA VOCHA;
Vocha hizi tunaweza kununua kupitia mitandao yote ya simu au kutoka apps za benki yoyote kwa kuweka namba ya malipo 6317897 jina linasoma WACHAGAWOTE TZ kama inavyoonekana kwenye picha zote mbili.
# Tafadhali hakikisha unaitunza meseji yako baada ya kufanya malipo kwakuwa ndio itakayotumika siku ya tukio Tarehe 30 Julai 2022




