Umoja wa Wachagawote ni nini?

 



Umoja Wa Wachagawote

Ni Umoja Wa Hiari Unaoundwa Na Wachaga Kutoka Old-Moshi, Machame, Kibosho, Marangu, Rombo, Siha Na Kwingine. 
...imeelezwa kwa kina soma zaidi

Lengo La Kuanzishwa Umoja Huu ni kusaidiana kijamii na kiuchumi 

#1  Kusaidiana Kijamii


Maswala Ya Kijamii Ni Pamoja Na Matatizo Mbalimbali Yatakayomfika Mwanaumoja Kama Vile Magonjwa, Misiba, Kuunguliwa Na Nyumba Na Kupatwa Na Mafuriko Na Mengine Yanayofanana Na Haya.



#2  Kusaidiana Kiuchumi

Kutaarifiana Fursa Mbalimbali Zilizopo Na Kupeana Mafunzo Ya Fedha Na Ukuzaji Wa Mitaji Na Kunyanyuana Kimaendeleo Kwa Kupeana Mikopo Nafuu Kama Vile Mikopo Ya Nyumba Na Viwanja Au Mikopo Kukuza Biashara. 
Faida Za Kuwa Mwanachama Wa Umoja Huu Zipo Nyingi Na Zitaendelea Kuongezeka Zaidi Hapo Badae Ila Kwa Sasa

Tumeelezea Chache Kwenye Ukurasa Wa About Us



Katika kuboresha mawasiliano ya Umoja wa Wachagawote tumejiunga kwenye mitandao ya kijamii ili kuweza kufikisha taarifa za Umoja huu kwa urahisi, ambapo kwa mtandao wa facebook tunao ukurasa unaitwa Wachagawote na mtandao wa twitter ukurasa wetu unaitwa Wachagawote pia kwa mtandao wa Instagram tunao ukurasa unaitwa Wachagawote na kwa mtandao wa Whatsapp tumeanzisha Group maalumu la wanachama hai ikiwa ni maboresho 

Kama inavyoelezewa vyema kwenye chapisho hili


 Hitimisho


Kwa maelezo haya mafupi tuna imani utakuwa umeelewa kiundani kuhusu Umoja wa Wachagawote na pia kwa kufatilia link zote zilizoambatanishwa kwenye chapisho hili utakuwa ujua zaidi kuhusu Taasisi hii ya Wachagawote


Ikiwa unahitaji ufafanuzi zaidi waweza kuwasiliana nasi kwa

kujaza fomu hii



Newer Post Older Post