Ripoti ya Kikao cha Wachagawote kilichofanyika Tarehe: 28 January 2024
1. Kufungua Kikao:
Kikao kilifunguliwa saa tisa jioni na Ndugu Mmary, na wanachama walikaribishwa.
2. Utambulisho:
Wanachama walijitambulisha kwa majina, makazi, na shughuli wanazofanya.
3. Mahudhurio
Kikao kilihudhuriwa na wanachama sita, kama ilivyoorodheshwa.
1. Patrick P. Lymo
2. Rizikiel Mmari (Mr. Ballo)
3. Anna W. Mushi
4. Justin A. Mbuya
5. Pascal P. Swai
6. Thadey Kitali
4. Uchaguzi:
Uchaguzi haukufanyika kutokana na uchache wa watu; Viongozi wa mpito watabakia hadi uchaguzi ujao utakaofanyika.
5. Katiba:
Wajumbe walipendekeza kuboresha katiba iliyopo ili kuendana na wakati uliopo na kuwa na tija kulingana na mipango tunayojiwekea ya sasa na baadae. Jambo hilo lilikubaliwa na litakalofanyiwa kazi kwa utaratibu maalumu tutakaouweka Wanachama hai kwa pamoja.
6. M-Koba Mpya:
Kutokana na wajumbe kuazimia kuwatambua Wanachama hai na wasio Wanachama hai, yalipitishwa maamuzi ya kuwa na KIINGILIO na pia kuwepo kwa ADA ya kila mwezi... Na ili kuweza kutunza fedha hizo wajumbe wakaamua kufunguliwa akaunti ya kikundi kupitia Mtandao wa Vodacom iitwayo M-Koba na ikafunguliwa pale pale kwa jina "WACHAGAWOTE GROUP" na wajumbe wote sita walijiunga rasmi na akaunti hiyo ya M-Koba siku hiyo hiyo.
7. Kiingilio na Ada:
Wajumbe walipendekeza kwa Mchaga yeyote anayependa kujiunga na Umoja huu wa Wachagawote na kuwa mwanachama hai ni sharti atoe kiingilio cha shilingi 50,000/= na pia awe tayari kulipa ada ya kila mwezi shilingi 10,000/=.
Viwango hivyo vitadumu kwa kipindi cha kuanzia Tarehe 28 January 2024 hadi Tarehe 30 Mei 2024 kwani ikifika Tarehe 01 June 2024 Viwango vitabadilika na kuwa kama ifutavyo;
- Kiingilio Tshs 100,000
- Ada kila mwezi Tshs 10,000
Na ieleweke kuwa Wanachama wanaotaka kujiunga baadae watalazimika kulipia ada za miezi yote tangu Tar. 01 February 2024 tulipoanzia.
8. Group Jipya la Whatsapp:
Kwakuwa tunatazamia kuwa na aina mbili ya Wachaga watakaungana nasi pamoja, Wajumbe walipendekeza kuundwa kwa group jipya kwa ajili ya wanachama hai peke yake ambao watakubali kufuata taratibu na sheria za kwenye katiba ya chama na kupata haki zote za uanachama hai. Group hilo litafunguliwa baada ya mwezi mmoja (Tarehe 01 March 2024)
9. Meeting Online:
Kutokana na hali ya maisha ilivyo na ukizingatia ufinyu wa muda wa kukutana mara kwa mara, hali ambayo itapelekea Wanachama wengi kukosa haki yao ya msingi kushiriki vikao vya chama, Wajumbe walishauri kufanya mikutano mtandaoni kwa wanachama hai tu ambayo mikutano hiyo itapitisha maamuzi ya chama na hata kupiga kura na kushiriki mada mbalimbali muhimu za chama.
Hata hivyo taarifa za mikutano inapaswa kutangazwa mapema ili wanachama hai wote waweze kushiriki na inapaswa kuheshimiwa na wanachama hai wote.
Mengineyo:
- Ili kuendelea kujenga msikamano na upendo baina yetu wanachama hai, Mwanzilishi Ndugu Mmari (Mr Ballo) aliomba utaratibu wa kutembeleana nyumba kwa nyumba uanzishwe na iwe ni kawaida yetu kama wanachama.
- Wajumbe walipendekeza taarifa zoote na matangazo yanayohusu umoja huu wa Wachagawote kama vile ratiba za kikao n.k. kutumwa kwenye group na kusisitizwa kwa nguvu zaidi ili kuwahamasisha wengine pia.
- Kama wanaumoja na wanafamili, endapo kutatokea mwenzetu amepatwa na tatizo atoe taarifa kwa uongozi na uongozi utaleta kwa wanachama kwa utaratibu maalumu kila mmoja aweze kutoa msaada kwa wanachama wakati wa shida na raha.
- Wajumbe waliazimia kuwepo na muda wa mwezi mmoja kila Mchaga mwenye nia ya kuwa Mwanachama hai kuwasiliana na Uongozi aweze kujiunga rasmi kwa kutoa Kiingilio na Ada ya kila mwezi.
Hitimisho:
Kikao kilifungwa saa 12:44 jioni na Mwenyekiti Ndg. Mmari (Mr Ballo) aliwashukuru wanachama kwa kuhudhuria na kuwasihi kuendeleza mshikamano na kuhakikisha tunasimamia utekelezaji wa yote tuliyoyaazimia pamoja.
Ripoti hii itatolewa kwa Wachagawote kwenye group itaruhusiwa kujadili na pia kutoa maoni zaidi. Ahsante kwa ushiriki wako.
