Muasisi wa Wachagawote ajibu tuhuma za utapeli...!

 

Baada ya hii leo Tarehe 7 February 2024 kujitokeza taaruki kwenye mtandao wa whatsapp kupitia magroup ya watumiaji wenye Asili ya Kichaga na haswa kwenye group ambalo limeanzishwa na Ndg. Mmari a.k.a Mr Ballo kwa kutajwa kujihusisha na Utapeli au udanyanyifu kwa wafuasi au wanachama wa makundi hayo yenye mkusanyiko wa members zaidi ya 2000 na kupelekea hofu kwa kiwango cha kufikia kuwagawa na mwisho kuhitajika ufafanuzi kuhusu shutuma hizo, hatimaye Muanzilishi wa WACHAGAWOTE amejitokeza na kuandika ujumbe huu hapa chini.



"Habari zenu wote👋🏾

Wachache mnanifahamu humu nami namshukuru Mungu kwa kunikutanisha nanyi mnaonifahamu na nawapenda sana nduguzangu. 

Wengi wenu mnalijua jina langu la Mr Ballo ambalo ni jina la kibiashara tu na sio jina la Kitambulisho au niseme jina la kubatizwa au nilipewa na wazazi wangu.

Jina langu halisi/nililopewa na Wazazi wangu ni RIZIKIEL ADAM MMARI. 

Mimi ni Mchaga Ukoo wa MMARI ya Old-Moshi na hapa Dar es Salaam ninaishi Kimara mwisho nikijishughulisha na utengenezaji wa matangazo ya biashara (Mabango, vipeperushi, stickers na vingine vyote vinavyohusu matangazo na printing) na pia nafanya Social media management pamoja na Digital Content creations(Mahudhui ya kimtandao).

Leo nimeamua kuweka wazi maelezo haya mafupi kuhusu mimi ili kuwapa nafasi wale wengi wetu wasionifahamu waweze kunifahamu na hata kuiona picha ya muonekano wangu halisi kwa ambao hawajawahi kuniona halisi.

Mimi ndio mwanzilishi wa kikundi cha Wachagawote, nilianzisha kurasa ya Facebook ya kwanza inayoitwa Wachagawote miaka takribani 8 iliyopita hadi kufikia mwaka juzi ilipodukuliwa na wahalifu wa kimtandao na sasa inatumwa mapicha machafu...

Hata hivyo baada ya kutumia wataalamu mbalimbali na kupoteza pesa nyingi kwa kuwalipa na mwishowe kushindwa kuirudisha niliamua kuanzisha nyingine kwa jina hilo hilo Wachagawote na hadi sasa ndio naisimamia huko Facebook na pia Instagram nilianzisha kurasa yenye jina hilo hilo la Wachagawote kwa kipindi cha miaka 7 sasa na bado naendelea kuisimamia mimi pia. Vile vile mimi ndiye nilianzisha group la Whatsapp linaloitwa Wachagawote na hadi leo hii mimi ndio Admin. Hii yote ni kwa lengo la kurahisisha Mawasiliano kati yetu sisi tulikutana kwenye hizo kurasa mbili za Facebook na Instagram. Naomba ikumbukwe kuwa vile vile nilianzisha kurasa za Wachagawote kwenye mitandao mingine pia kama Twitter na Tiktok ili kukuza wigo wa Mawasiliano kwetu kidigitali.



Naomba nimalize kwa kuthibitisha kuwa mimi Mr Ballo (Rizikiel Mmari) sijihusishi na wala sijawahi kuanzisha michezo ya kukopeshana hela au kuchangishana hela kwa namna yoyote ile kama ilivyoelezwa kwenye baadhi ya magroup mengine ya whatsapp ya Wachaga na hali hiyo ikajitokeza pia kwenye group la WACHAGAWOTE ambalo mimi ndio mwanzilishi na pia imefika mbali na kuhisiwa au kutajwa kwenye kashfa ya Utapeli wa mtandaoni hali inayopelekea baadhi kupata hofu kuhusiana na akaunti ya M-Koba niliyoianzisha mimi kama Admin wa Group la Wachagawote kwa lengo la wanachama hai kujiwekea pesa za kiingilio elfu 50 na ada ya kila mwezi elfu 10.

Natumia nafasi hii kuomba radhi wale waliopata ukakasi, usumbufu au kadhia yoyote ile kuhusu Majina yangu au taarifa zozote zile zilizopotoshwa kuhusu mimi na kuchanganywa na hao waasisi wengine kwenye makundi Mengineyo ambayo mimi sihusiki na nimekuwa nikiyasikia tu bila kujua uhalisi au uhalali wake na jinsi yanavyopelekea mimi kuhusiswa nayo.

Naomba nimalizie kwa kushukuru wote kwa kusoma ujumbe huu na nina imama kila aliesoma ataelewa na kama kutakuwa na maswali naomba mniulize hapa hapa ntayajibu. Asante

Taarifa hii imeandikwa na Rizikiel A. Mmari  (Mr. Ballo) ambaye ni Admin na Mwasisi wa Umoja wa Wachagawote."

Newer Post Older Post